Exclusive: Picha 20 kutoka kwenye Sherehe ya Kuzaliwa ya Malkia Elizabeth wa Uingereza #share Waziri Mkuu wake hakuhudhuria...
Malkia Elizabeth wa Uingereza, leo alivunja miiko ya sherehe yake ya siku ya kuzaliwa kwa kuchapisha waraka akiwataka Waingereza popote walipo kuwatakia faraja wenzao walioathirika kwa namna moja na kupoteza ndugu kwenye shambulizi la Manchester Arena lililopoteza maisha ya watu 22, na tukio la moto la Grenfell Tower ambapo watu 30 wamethitika kufariki na wengine 70 hawajulikani walipo..
Mbali na Gwaride la kimyakimya lilihudhuriwa pia na Prince Phillip, kivutio kikubwa kilikuwa ni kitendo cha Prince Charles na mwanawe Prince William, waliopamba sherehe hiyo wakiwa kwenye mavazi maalum ya kifalme yenye vyeo vya kijeshi huku wakizunguka uwanja kwa mbio za farasi kusambaza salamu za upendo za Malkia ambae tayari amepindukia miaka 90.
Katika Waraka huo ambao Matukio imetumiwa nakala yake, Malkia alisema.. "..ni kweli siku ya leo ni siku kubwa ya kitamaduni kwa Taifa letu, lakini hali ya nchi ipo kwenye mtihani mkubwa.. tumeshuhudia misururu ya majanga, na hatuwezi kwenda tofauti na hali hali ya mioyo yetu kwa sasa" ulimalizia waraka huo wenye ukurasa mmoja..
Kwa mara ya kwanza, Kinyume na tamaduni za Uingereza, kwenye sherehe hizo alikosekana Waziri Mkuu ambae ndie mhusika mkuu kwenye kamati ya maandalizi.. ambapo Bibi Theresa May amelazimika kwenda kuongoza kikao maalum cha maafa kuashiria uzito wa hali ya sasa ya Uingereza..
No comments:
Post a Comment