Ona LHRC 'ilivyoichimba biti' EWURA,.. #SHARE .. ni kuhusu kuiongezea muda IPTL!!


Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimepinga kusudio la Ewura la kutaka kukusanya maoni ya wananchi ili kuiongezea muda leseni kampuni ya IPTL. Akizungumza leo ofisini kwake Jijini Dar Es Salaam, Mkurugenzi wa LHRC Anna Henga amesema maoni hayo yasifanyike hadi serikali itakapotekeleza  mapendekezo yaliyotolewa na Bunge mwaka 2014.
Bi Anna amefafanua kwamba,  mapendekezo hayo ni pamoja na Takukuru kufanya uchunguzi kuhusu umiliki na uwepo wa rushwa ndani ya IPTL na wadau wake. Amesema,  mapendekezo yaliyotolewa hayajafanyiwa kazi huku umma wa watanzania ukiwa hauelewi kinachoendea.
LHRC itasimama kidete kuipinga kampuni ya IPTL hasa baada ya kuibuka kwa sakata la akaunti ya ESCROW. Amewataka Watanzania waipinge kampuni hiyo kwa kwa nguvu moja kwa sababu ndiyo chanzo cha ongezeko mara kwa mara kwa bei ya umeme.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search