Usajili Mpya: Habari njema kwa Mbeya City.. 'Samatta' asema yuko tayari kwa mazungumzo !! #share

Katika jitihada za kusogeza vikombe vingi klabuni msimu ujao.. Timu ya wakusanya ushuru ya Mbeya City tayari inamuwinda mshambuliaji nguli wa Prisons, Mohamed Samatta ili kuimarisha kikosi chake.

Samatta tayari imefanya mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya na Prisons ingawa mwenyewe amesema mazungumzo hayo hayamzuii kupokea ofa nyingine.


Kocha wa Mbeya City, Mmalawi Kinnah Phiri alipendekeza usajili wa Samatta ambapo alisema kuwa mchezaji huyo atasaidia kuziba pengo la Kenny Ally aliyesajiliwa na Singida United kwa madai ya kwamba uwezo wao kisoka unafanana.

Samatta msimu uliopita ameifungia Prisons mabao matano katika Ligi Kuu Bara.

Samatta alisema mkataba wake na Prisons ulikuwa wa mwaka mmoja, amefanya mazungumzo na viongozi ambapo anaamini kwamba watafikia muafaka na anafurahia maisha ya hapo kwa kipindi chote alichoishi na Prisons.

"Kuhusu Mbeya City pengine wao wameniweka kwenye mipango yao ila bado hawajaniambia jambo lolote, nimemaliza mkataba na Prisons tumezungumza ila bado hatua ya mwisho hivyo sizuiliwi kupokea ofa kutoka timu nyingine kwani mimi ni mchezaji huru."

Source: QO

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search