sPORTS nEWS: Simba yaanza kwa kichapo Afrika Kusini...#share

Klabu ya Simba imechezea kichapo cha goli 1-0 kutoka kwa klabu ya Orlando Pirates katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye dimba la Orlando nchini Afrika Kusini.



Goli hilo ambalo lilifungwa mnamo kipindi cha kwanza limeweza kudumu hadi mwisho wa mchezo na hivyo Simba kuambulia patupu.

Kwa zaidi ya majuma matatu sasa klabu ya Simba ipo nchini Afrika kusini kwa maandalizi ya mechi ya Simba day, Ngao ya Jamii dhidi ya watani wao wa jadi Yanga pamoja na msimu ujao wa Ligi kuu Tanzania Bara.


Na huo ni mchezo wa kwanza wa kirafiki kwa klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi ikiwa Afrika Kusini na Mchezo wa pili inatarajiwa kupepetana na klabu ya Bidverst.


Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search