Abiria watakiwa kuwapeleka Polisi wanaopandisha nauli kiholela...soma habari kamili na matukio
Na Salha Mohamed,Dar es
Salaam
BARAZA la Ushauri na
Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Nchi Kavu na Majini, limewataka wananchi
kutoa taarifa kwa mamlaka husika ikiwamo Polisi endapo watatozwa nauli tofauti na
zilizopangwa.
Hatua hiyo inafuatia katika kipindi hiki cha mwezi Desemba nauli hasa kwa wasafiri waendao mikoani wanaotumia usafiri wa mabasi hupanda maradufu.
Katibu Mtendaji ,Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Nchi kavu na Majini, Dk. Oscar Kikoyo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya usafiri ilivyo katika kipindi hiki cha sikukuu za Krismas na Mwaka Mpya wa 2018.
Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na katibu mtendaji wa baraza hilo, Dk Oscar
Kikoyo wakati akizungumzia hali ya usafiri katika kipindi cha sikukuu za
krismas na mwaka mpya (2018).
"Baadhi ya watoa huduma
ambao si waaminifu katika kipindi hiki kama ni njia ya kuvuna zaidi kutoka kwa watumiaji
kinyume na masharti ya leseni zao. Hivyo wasafiri wachukue hatua ya kuwapeleka
polisi au katika mamlaka husika za usafirishaji, "amesema.
Amesema kutokana na mahitaji
makubwa ya usafiri, baadhi ya abiria hukubali kulipa zaidi ili wapate kusafiri.
Dk. Kikoyo ameukumbusha
Umoja wa wamiliki wa mabasi yaendayo
mikoani(Taboa),kufuata masharti ya leseni zao na kutoza nauli zilizoidhinishwa
na Sumatra.
"Baraza linawahimiza
wamiliki, kuwahimiza wafanyakazi wao wanaokata tiketi katika vituo mbalimbali
kuwa waaminifu kwa waajiri na wateja
wao,"amesema.
Amesema wananchi wasinunue
tiketi kwa wapiga debe au vishoka katika kituo cha mabasi Ubungo au vituo
vingine pamoja na kuhakikisha jina na kiwango sahihi alichotoa na
kilichoandikwa.
Ameongeza magari yaliyopewa
vibali vya muda kusafirisha abiria mikoani yakaguliwe kwa kina kabla ya kukata
tiketi.
Kuhusu wanaobeba mizigo
katika vitua vya mabasi amesema ‘’ Kwanza mkubaliane bei kabla hajabeba
mizigo pia akupe au akuonyesha kadi yake
yenye namba iliyoandikwa kwenye koti lake nyuma, mbele na kwenye toroli lake.’’
No comments:
Post a Comment