Waziri Jafo ateta na wakuu wa wilaya...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
WAKUU wa Wilaya nchini wameagizwa kusimamia  kazi zinazofanywa na Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (Tarura)  ili kuleta matokeo tarajiwa  katika kukuza ustawi wa uchumi nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo katika kikao cha  Wakuu wa Wilaya kuhusiana na  kujenga uelewa wa majukumu ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini(Tarura) katika ukumbi wa Hazina Dodoma.
Agizo hilo limetolewa leo mjini Dodoma na waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Suleimani Jafo akifungua kikao cha wakuu wa wilaya nchini.
Jafo amesema “Nawaagiza wakuu wa wilaya nchini kote muende kusiamamia barabara hizo kwa ukaribu ili barabara zitakazo jengwa ziwe na ubora na zitakazo dumu kwa muda mrefu,”.
Amewaambia viongozi hao kuwa uanzishwaji wa Tarura utainua chachu ya
uzalishaji wa mazao kutokana na usafiri wa uhakika kwani mkulima atakuwa na uhakika wakusafirisha mazao, lakini pia itapunguza gharama za
usafiri na kuboresha hali za maisha za watanzania.


Ameeleza kwamba serikali imekuwa na changamoto kubwa ya wakandarasi  wanaopatiwa kazi za ujenzi wa barabara kutokuwa waaminifu na kujenga chini ya kiwango, rushwa , hivyo ni kazi ya mkuu wa Wilaya kusimamia ili kubaini mapungufu hayo kwa haraka na kuokoa fedha za Serikali.
Amesema kuwa baada ya kuifahamu Tarura ni jukumu lao kuibua maovu kwa wafanyakazi wanaofanya maovu ili waweze kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kufuata sheria na taratibu za utumishi wa umma.
Amesema kuwa Wakuu wa Wilaya ni wawakilishi wa serikali katika maeneo yao, hivyo wanawajibu wa kusimamia kwa ukaribu zaidi katika usimamizi wa
mradi ya Ujenzi wa Barabara nchini.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search