Mtulia atoa la moyoni, aenda kulima Rufiji...soma habari kamili na matukio360..#share
Na mwandishi wetu
SIKU mbili baada ya
kujiuzulu ubunge, kung’atuka CUF na leo kujiunga CCM, Maulid Mtulia amesema
yeye ni mwanajeshi na yupo tayari kwa kazi yoyote atakayopewa na chama hicho,
ikishindikana atakwenda kulima kijijini kwao wilayani Rufiji.
Maulid Mtulia akionyesha kadi yake ya CCM mara baada ya kujiunga na chama hicho hii leo jijini Dar es Salaam
Akizungumza katika mahojiano
maalum na matukio360 hii leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kujiunga CCM
amesema hawezi kukubali au kukataa kama atagombea tena ubunge katika jimbo hilo.
"Elewa mimi ni
mwanajeshi nipo tayari kufanya kazi yoyote ndani ya CCM. Kama nitagombea ubunge
ama la, muda wa hilo bado. Kutangaza nia kuna muda wake,’’ amesema Mtulia
Amesema hata kama CCM
haitompa kazi ya kufanya atakwenda kijijini kwao katika wilaya ya Rufiji kulima.
“Hata kama CCM haitonipa kazi ya kufanya nitakwenda
kwetu Rufiji kulima,’’ amesema
Awali baada ya kukabidhiwa kadi Mtulia amesema:
"Nimejivua nyadhifa zangu zote ya Ubunge wa
Kinondoni na vyeo vyote nilivyokuwa navyo CUF na kuamua kujiunga na CCM
kutokana na kuridhishwa na CCM ya sasa na utendaji wa Rais Dk. Magufuli"
"Mimi ni mgeni na salamu ninayoijua ya CCM ni CCM
Oyeee"
"Nimejiunga na CCM ili
kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na Rais Dk. Magufuli"
"Nimetoka kwenye chama
chenye migogoro mingi, nimekuja kwenye chama chenye amani, haki na Demokrasia
ya kweli"
"Ningekuwa Mbunge
kupitia CCM ningefanya mengi makubwa zaidi"
"Sijaja CCM kutafuta
cheo bali nimetumia haki yangu ya kidemokrasia ya kujiunga na chama chochote
kile ninachokitaka"
"Kila jambo nililokuwa
namwomba Rais tena hadharani (mfano wakati wa ufunguzi wa maghorofa)
ameyatekeleza kwa kiwango kikubwa" -
"Nawashangaa Viongozi
wa Upinzani wanaopinga na kususa mambo ya Serikali na shughuli za Bunge, hizo
shida za Wananchi Nani atawatatulia endapo wanawasusia wenye mamlaka?"
"Nipo tayari kuwa hata
Balozi wa nyumba kumi na ikishindikana nitaenda kuvua samaki nyumbani
Rufiji" - Mtulia
"Nawahaidi wana CCM
watafurahia uwepo wangu na watanufaika nami ndani ya CCM"
"Nawaambia wana Kinondoni wasikosee, wachague
Mbunge anayetokana na CCM. Wachague CCM siku zote" -
No comments:
Post a Comment