Jeshi la Tanzania, Rwanda waunganisha nguvu...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Hussein Ndubikile
JESHI la polisi nchini
limeingia makubaliano ya kuunganisha nguvu na kushirikiana katika kupambana na kudhibiti
uhalifu wa mtandaoni na jeshi la polisi la Rwanda.
IGP, Simon Sirro
Hayo yamesemwa leo jijini
Dar es Salaam na Inspekta Jenerali wa jeshi hilo IGP, Simon Sirro alipokutana na
mkuu wa Jeshi la Polisi la Rwanda, Emmanuel Gasana kuangalia utekelezaji wa
makubaliano yaliyoingiwa na majeshi hayo mwaka 2013.
Amesema kutokana na jeshi
hilo kuwa na uzoefu wa kupambana na uhalifu wameona ni vyema wakaungana nalo
kubadilishana na kupata mbinu madhubuti ya kuwakamata wahalifu na wanaendelea
kushirikiana kupambana na dawa za kulevya kwa kufanya operesheni za pamoja
mpakani mwa nchi hizo.
" Tunakwenda vizuri
kwani kati ya makubaliano tuliyoingia kipindi cha nyuma yametekelezwa ipasavyo
nawaeleza wahalifu ambao wako Rwanda na Tanzania hawako salama watafute
shughuli nyingine ya kufanya tutawakamata na watafikishwa mbele ya vyombo
husika," amesema Sirro.
Amesema lengo la ushirikiano
kiulinzi ni kuhakikisha wananchi wanaishi katika hali ya amani na utulivu na
wataalam watatoka nchini kwenda Rwanda kupata uzoefu wa kukabiliana na uhalifu
huo wa kimtandao.
No comments:
Post a Comment