Mbunge wa Kinondoni ajiuzulu ubunge ...soma habari kamili na matukio360..#share

Na mwandishi wetu
MBUNGE wa jimbo la kinondoni jijini Dar es Salaam(CUF), Maulid Mtulia  hii leo ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo.
Aliyekuwa Mbunge wa kinondoni kwa tiketi ya CUF, Maulid Mtulia.

Taarifa yake kwa vyobo vya habari inaeleza kuwa:
"Mimi Maulid Said Abdallah Mtulia Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF) kwa hiari yangu nimeamua kujiuzulu uanachama wa CUF na kujiuzulu nafasi zake zote za uongozi nilizokuwa nashikilia.

Nimefanya uamuzi huu leo tarehe 02/12/2017 kwa utashi wangu na bila  shinikizo la mtu yeyote.

Sababu za kufanya hivi ni kutokana na uzoefu nilioupata kwa miaka miwili ya ubunge wangu ambapo nimebaini kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho ni chama tawala inafanya kazi kubwa ya kutekeleza Ilani na imefanya vizuri katika mambo mengi ambayo sisi upinzani tuliahidi kuyatekeleza.

Kwa kuwa nia yangu ni kuwatumikia wananchi, sioni sababu ya kuendelea kuwa upinzani na badala yake nimeona ni vema niungane na juhudi za Serikali kwa kumuunga mkono Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi maendeleo na kukabiliana na kero mbalimbali.

Nawashukuru wananchi wa Jimbo la Kinondoni kwa kunipa dhamana ya ubunge katika uchaguzi mkuu uliopita na nawaahidi kuwa nipo tayari kuendelea kushirikiana nanyi katika maendeleo nikiwa katika uwanja mwingine wa siasa ambao ni Chama Cha Mapinduzi.

Pia nawaomba wananchi na viongozi wengine ambao wanatambua mchango wa Rais Magufuli na Serikali yake kutosita kuungana nae katika kazi za kuitumikia nchini badala ya kuwa wapinzani."




About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search