Senegal wataka kufika nusu fainali kombe la Dunia...soma habari kamili na matukio360...#share
Na mashirika ya kimataifa
WAZIRI wa michezo wa
Senegal, Matar Ba amesema timu ya taifa ya nchi hiyo itafanya vizuri zaidi
katika michuano ya kombe la dunia zaidi ya taifa lolote la Afrika, kwa kufika
nusu fainali ya michuano hiyo itayofanyika nchini Urusi mwakani.
Timu ya taifa ya Senegal
Mwaka 2002 kwa mara ya
kwanza Senegal iliposhiriki michuano hiyo ilifanya vyema kwa kufika hatua ya
robo fainali, Simba wa Teranga wamepangwa katika kundi H, na wakiwa na timu za
Poland, Colombia na Japan.
"Tunapaswa kuwa na
malengo yetu - malengo hayo ni kufikia nusu fainali na kufanya vizuri kuliko
mwaka wa 2002," Waziri huyo aliiambia BBC.
Waziri Ba akasisitiza kwa
kusema "Tuna timu nzuri na bora na tuna kocha wetu raia wa Senegal na
tutajitayarisha vizuri kwa ajili ya kwenda kufanya vizuri.
Mchezo wa kwanza wa Senegal
watacheza na Poland, June 19 kisha watacheza na Japan June 24, na watamaliza
kazi kwa mchezo wa tatu kwa kukipiga na Colombia
No comments:
Post a Comment