Watano wafariki, 11 wajeruhiwa...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
WATU watano wamefariki na 11 wamejeruhiwa katika ajali kumi tofauti zilizotokea katika siku ya Krismass
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani SACP Fortunatus Musilimu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi
Kikosi cha Usalama Barabarani SACP Fortunatus Musilimu akizungumza na waandishi
wa habari alipokuwa akitoa taarifa ya tathimini ya hali ya ajali za barabarani
nchini kuelekea mwishoni mwa mwaka 2017 na mwanzoni mwa mwaka 2018.
“Sikukuu ya Krismasi ya mwaka jana (2016) kulitokea jumla ya
ajali 14 zilizosababisha vifo 10 na majeruhi 15, zinabainisha kuwepo kwa
upungufu wa ajali 4 ambazo ni sawa na asilimia 29, upungufu wa vifo 5 ambavyo
ni sawa na asilimia 50 na upungufu wa majeruhi 4 ambao ni sawa na asilimia 27,”
amesema SACP Musilimu.
Amesema hata katika sikukuu ya kufungua zawadi (Boxing Day)
Desemba 26, 2017 kulitokea ajali 6 nchini ambazo zilisababisha vifo 4 na
majeruhi 8.
Ameeleza kuwa takwimu hizo zikilinganishwa na kipindi kama
hicho kwa 2016 ambapo kulitokea ajali 6, vifo na majeruhi 9 zinabainisha
kutokuwepo kwa ongezeko au upungufu wa ajali, kuwepo kwa upungufu wa kifo
kimoja ambacho ni sawa na asilimia 20 na upungufu wa majeruhi mmoja ambaye ni
sawa na asilimia 11.
SACP Musilimu ameongeza kuwa kuanzia Desemba 19, 2017 hadi
Desemba 25, 2017 wiki moja kabla ya sikukuu ya krismas kulitokea ajali 42, vifo
46 na majeruhi 46.
Amesema takwimu hizo zikilinganishwa na kipindi kama hicho
mwaka jana ambapo kulitokea ajali 55, vifo 52 na majeruhi 75 zinabainisha
kuwepo kwa upungufu wa ajali 13 ambazo ni sawa na asilimia 24, upungufu wa vifo
6 ambavyo ni sawa na asilimia 12 na upungufu wa majeruhi 30 sawa na asilimia
39.
Amesema katika kipindi hiki ajali zimekuwa zikisababishwa na
mwendo kasi, kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari (Overtaking),
ulevi na magari mabovu.
Amewataka madereva kuhakikisha wanazingatia sheria
wanapoendesha vyombo vya moto kwani ambao watakaidi watashurutishwa lakini pia
watakamatwa na kuwekwa mahabusu na kisha kuwapeleka mahakamani pamoja na
kuwafungia leseni zao wakitoka.
No comments:
Post a Comment