HESLB kuwasaka wadaiwa mikopo elimu ya juu...soma habari kamili na matukio360...#share
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HESLB) imesema
itaanza kuwasaka wanufaika 119,497
nchini ambao wamekiuka sheria ya kuanza kurejesha mikopo yenye thamani ya
sh.bilioni 285.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo nchini (HSLEB) Abdul-Razaq Badru, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam
alipokuwa akitoa tathmini ya utekelezaji ya majukumu ya bodi kwa mwaka wa fedha
2017/2018 ulioshia Desemba 31, 2017.
“Wanufaika hao ni wakuanzia mwaka 1994 hadi 1995 tutaanza kuwasaka
kuanzia jumatatu januari 8, 2018,”amesema.
Amefafanua kuwa “Tutaanza kukagua taarifa za mishahara za waajiri
(payroll) ili kubaini waajiri ambao wanawasilisha kiwango kidogo cha mikopo ya
wafanyakazi wao ambao ni wanufaika pamoja na waajiri ambao hawawasilishi kabisa
pesa hizo kwenye bodi hiyo kwa mujibu wa sheria ili wachukuliwe hatua stahiki,”amesema.
Amesema katika msako huo hawatamwacha mtu au mwajiri atakayekiuka sheria
iliyoanzishwa na bodi na kufafanua kuwa sheria hiyo inatoa mamlaka ya kufanya
ukaguzi na ni kosa kisheria kwa mtu yeyote kuzuia ukaguzi huo.
Amesema hadi Desemba 31,2017 sh bilioni 85 zilikusanywa huku lengo la
makusanyo kwa mwaka mzima wa fedha utakaomalizika June 30 ,2018 ikiwa sh
bilioni 130.
“Katika kazi
hii ya ukusanyaji wa mikopo miezi hii sita tumewabaini wanufaika wapya 26000 na
wameanza kulipa na kufanya jumla ya waliolipa kuwa zaidi ya sh
121,000,”amesema.
No comments:
Post a Comment