Samia Suluhu atoa pole kifo mke waziri Lugola...soma habari kamili na matukio360...#share


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Kangi Lugola alipofika kutoa pole ya msiba wa mke wake, Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola aliyefariki siku ya tarehe 01, Januari, 2018 katika hospitali ya Rabininsia jijini Dar es Salaam

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa mke wa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Lugola, Kamishna Msaidizi wa Polisi marehemu Mary Lugola aliyefariki siku ya tarehe 01, Januari, 2018 katika hospitali ya Rabininsia jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiifariji familia ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Kangi Lugola wakati alipoenda kuwapa pole ya msiba wa Kamishna Msaidizi wa Polisi marehemu Mary Lugola nyumbani kwao klabu ya reli, Gerezani, jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Kangi Lugola wakati alipoenda kutoa pole ya msiba wa mke wake Kamishna Msaidizi wa Polisi marehemu Mary Lugola aliyefariki siku ya tarehe 01, Januari, 2018 katika hospitali ya Rabininsia jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwapa pole watoto wa  marehemu Mary Lugola , aliyekuwa mke wa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira  Kangi Lugola aliyefariki siku ya tarehe 01, Januari, 2018 katika hospitali ya Rabininsia jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa msibani kwa Kamishna Msaidizi wa Polisi marehemu Mary Lugola mke wa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira  Kangi Lugola, wengine pichani ni Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais  January Makamba (wa kwanza kushoto), Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo (wa pili kulia) na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais  Butamo Phillip.

Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search