Mkuu wa mkoa awasainisha mkataba wakuu wa wilaya....soma habari kamili na matukio360..#share

Na mwandishi wetu, Mbeya

MKUU wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amewasainisha  mkataba wakuu wa wilaya ili  watekeleze ujenzi wa vituo vya  afya na zahanati 453  katika kata na vijiji  kwa kipindi cha mwaka 2018/2020.
Amos Makalla

Mikataba hiyo imesainiwa leo mara baada ya kikao kazi cha kujadili
changamoto katika sekta ya afya kilichohusisha wakuu wa wilaya,
wakurugenzi wa halmashauri, waganga wakuu ,watendaji wa ngazi za kata na vijiji, na kwamba mikataba  hiyo itapelekwa kwa Waziri wa Afya,  Maendeleoya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto,  Ummy Mwalimu.

Amesema kuwa amelazimika kufanya hivyo  kutokana na mwamko duni wa ujenzi wa vituo vya afya na zahanati jambo  linachangia jamii kukosa
huduma za  afya ya msingi

"Wakuu wa wilaya hiki ni kipimo, utendaji wa kazi  ni jambo la
kushangaza mkoa una  vijiji 533 lakini vilivyo na  vituo vya afya ni
233 sawa na asilimia 34.7 ambapo vijiji 300 havina huduma ya afya ,
wakati kuna kata 174 na  zahanati zilizopo ni 25 kata 157 hazina   kwa
kweli katika hili sitovumilia,"amesema Makalla

Makalla amesema  watendaji wa serikali wanatakiwa kutambua sera inaelekeza nini katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.

Mwenyekiti wa wakuu wa wilaya , mkuu wa wilaya ya Chunya, Rehema
Madusa amesema  watatekeleza haraka makubaliano ya mikataba hiyo kwa kuhakikisha wanatumia mapato  ya ndani katika halmashauri na fedha zinazotoka serikalini  ili ifikapo 2020  vituo vya afya na zahanati
vikamilike.


Mwenyekiti wa wakurugenzi wa halmashauri, Sophia Kumbuli amesema kuanzia sasa wataweka vipaumbele katika kutekeleza  sera ya serikali kuwekeza katika sekta ya afya  ili kuhakikisha changamoto ya upungufu vituo vya afya na zahanati inapungua.

Kaimu mganga mkuu wa  mkoa, Yahya Msuya ametoa wiki  mbili kwa wakuu  wa wilaya na wakurugenzi kuandaa mpango kazi  na  kwamba uamuzi wa mkuu wa mkoa  utasaidia kuboresha huduma za afya na idadi kubwa ya wananchi kupata huduma bora na salama.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search