Kesi ya Lissu yaunguruma mahakama ya Kisutu...soma habari kamili na matukio360..#share


 Na Abdulrahim Sadiki, Dar es salaam
KESI  inayomkabili mwanasheria mkuu wa  Chadema,Tundu Lissu na wahariri wa gazeti la Mawio katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirishwa hadi Februari 26,2018.

Tundu Lissu
Leo wakili wa serikali, Elia Athanas alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba  kesi imepangwa kwa ajili ya kutajwa na kwamba hadi sasa hawajajua hali ya mshtakiwa wa nne Lissu.

Hivyo ameomba kesi hiyo ipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa na Hakimu Simba ameiharisha hadi Februari 26,2018.

Kesi hiyo ipo katika hatua ya usikilizwaji wa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka inamkabili Lissu ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki na wenzake  Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh.

Kwa pamoja washtakiwa hao, wanakabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.

Inadaiwa kuwa Januari 12 hadi 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam, washtakiwa watatu, Jabir, Mkina na Lissu, kwa pamoja waliandika na kuchapisha taarifa‎ za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar’.

Katika shtaka la pili wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam,  walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.

Mshtakiwa Mehboob anadaiwa kuwa Januari 13,2016 katika jengo la Jamana lililopo Manispaa ya Ilala,  Dar es Salaam, alichapisha gazeti la Mawio lililokua na taarifa za uchochezi.

Inadaiwa kuwa mshtakiwa huyo pia alichapisha gazeti hilo bila ya kuwasilisha hati ya sheria ya kiapo kwa Msajili wa Magazeti.
Mbali na mashtaka hayo washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016,  Dar es Salaam, bila ya kuwa na mamlaka yoyote, waliwatisha na kuwatia hofu wananchi wa Zanzibar  wasiweze kuingia kwenye marudio ya Uchaguzi Mkuu.
mwisho

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search