Meya Ubungo, Temeke wazichapa kavukavu....soma habari kamili na matukio360..#share

Na Salha Mohammed, Dar es salaam

WAZICHAPA kavukavu ndivyo unavyoweza kusema baada ya meya wa Ubungo(Chadema) Boniface Jacob na meya wa Temeke(CCM) Abdallah Chaurembo leo kupambana hadharani katika uchaguzi wa naibu meya wa jiji la Dar es salaam.


Meya wa Ubungo na wa Temeke wakiamuliwa baada ya kupambana kavukavu leo jijini Dar es salaam katika ukumbi wa karimjee katika uchaguzi wa naibu meya wa jiji la Dar es salaam.

Hatua hiyo ilifuatia baada kuibuka kwa mvutano wa wajumbe wa Baraza la jiji wa CCM na Ukawa ambapo Ukawa walitaka uchaguzi huo kuahirishwa kufuatia mgombea wao kuwa mgonjwa huku CCM wakipinga.

Hata hivyo uchaguzi ulifanyika na mkurugenzi wa jiji Sipola Liana alimtangaza Musa Kafana(CUF) kuwa mshindi kwa kupata kura 12 kwa kumi za  Mariam Mrolida (CCM) na kwamba  hakuna kura zilizoaribika.

Jiji la Dar es salaam linaongozwa na meya Isaya Mwita(Chadema)

Angalia picha mbalimbali zikionyesha matukio yaliyoajiri katika ukumbi wa karimjee jijini Dar es salaam. Picha zote na Salha Mohammed


Hhhhhhhhhh
Mgombea wa Ukawa, Musa Kafana akiwa amebebwa kuingia katika ukumbi wa karimjee


Zzzzxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx



Musa Kafana akiwa amelala

Musa Kafana akiwa amefunikwa joho

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search