Uminywaji uhuru kujieleza LHRC kushtaki kimataifa...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Abraham Ntambara,Dar es Salaam
KUTOKANA na mbano wa uhuru wa kujieleza nchini, Kituo cha
Sheria na Haki za Binadam (LHRC), kimesema kinampango wa kushtaki suala hilo
kwenye vyombo vya kimataifa vinavyohusika na uangalizi wa haki za binadamu.
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Dk. Helen Kijo-Bisimba, akizungumzi na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Msimamo huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi
Mtendaji wa LHRC Dk. Helen Kijo-Bisimba akizungumza na waandishi wa habari siku
moja baada ya ya Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kuvitoza vituo vitano vya
televisheni faini ya sh. milioni 60.
“Tumeshuhudia serikali kupitia TCRA ikitoa adhabu
kwa vituo vitano vikubwa vya luninga ambavyo nia Azam TV, ITV, Channel 10, Str
TV na EATV kwa kile kinachodaiwa kuwa ni ukiukwaji wa kanuni ya maudhui 2005
baada ya televisheni hizo kurusha habari kuhusu tathmini ya haki za binadamu
katika uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika Novemba 2017 iliyotolewa na LHRC,”
amesema Dk. Kijo-Bisimba.
Ameongeza “LHRC imechukua hatua ya kutoa taarifa kwa vyombo
vya kimataifa vinavyohusika na uangalizi wa haki za binadamu kuomba waingilie
kati suala la uhuru wa kujieleza nchini,”
Dk. Kijo-Bisimba amesema kufuatia hatua hiyo ya TCRA, LHRC
imechukua hatua nyingine nne za kufanya ambazo ni kuandika barua TCRA kuwataka
kufanya semina kwa kituo hicho na taasisi nyingine juu ya namna bora ya kuandaa
maudhui.
Nyingine ni kuungana na wadau ambao wako tayari kwenda
mahakamani kuomba tafsiri ya neno UCHOCEZI na baadhi ya vifungu vya kanuni ya
maudhui hususani kifungu namba 8 katika mazingira ya utawala wa serikali dhidi
ya raia.
Kimeanzisha harambee ya kuchangia gharama ya kuvisaidia
vyombo vya habari vilivyokumbwa na adhabu pamoja na kuitaka serikali ya awamu
ya tano kuheshimu katiba iliyopo kwa kutoingilia uhuru wa kujieleza.
Kwa mujibu wa kamati ya maudhui ya TCRA, vyombo hivyo
vimetiwa hatiani kwa makosa matatu chini ya kifungu cha 5 na 6 vya kanuni za
maudhui za mwaka 2005 na kupigwa faini kwa viwango tofauti pamoja na kuwekwa
chini ya uangalizi kwa miezi sita.
No comments:
Post a Comment