Tanzania yapata tuzo kimataifa...soma habari kamili na matukio360..#share

Na Salha Mohamed,Dar es salaam


TANZANIA imepata tuzo ya kimataifa ya utekelezaji wa sera za mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza pamoja na dola 5,000 kupitia taasisi za kiraia.

Kaimu Mkurugenzi magonjwa yasiyoambukiza, wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Sarah Maongezi (kushoto) akimkabidhi tuzo ya kimataifa Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya magonjwa yasiyoambukiza (TANCDA), Dk Tatizo Waane.

Tuzo hiyo ya mwaka 2017 imetolewa na Shirikisho la Kimataifa la Magonjwa yasiyoambukiza (Global NCDs Alliance) kwa kushirikiana na Falme za kiarabu za mji wa Sharja.


Kaimu Mkurugenzi Magonjwa yasiyoambukiza, Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Sarah Maongezi amesema magonjwa yasiyoambukiza husababisha asilimia 27 ya vifo vyote  nchini.


"Taasisi changa ya waandishi wanaopambana na magonjwa yasiyoambukiza (TJNCDF) imefanikiwa kuchochea elimu hii, hivyo sina budi kuipongeza, "amesema.


Amesema magonjwa yasiyoambukiza kama moyo, mishipa ya damu, kisukari, saratani, pumu, figo, ini, macho, meno ni moja ya sababu za tishio la uhai wa binadamu duniani ambayo yanatokana na tabia za mienendo na ulaji mbaya.


"Magonjwa haya huwapata watu ambao hawashughulishi miili yao kwa kazi za kutoa jasho na mazoezi, wanaokula kwa wingi vyakula vya mafuta, sukari, chumvi na wanga hasa katika umri wa utu uzima zaidi ya miaka 30.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha wenye Kisukari, Profesa Andrew Swai amesema TJNCDF wanapaswa kujua wamefikia watu wangapi na wangapi wamebadilika kutokana na elimu waliyopata.



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search