Bilioni moja kununua mashine ya vinasaba....soma habari kamili na matukio360....#share

Na Mwajuma Juma, Zanzibar
SHILINGI bilioni moja zimetengwa kununua mashine ya kuchunguza vinasaba DNA visiwani Zanzibar.

Mahmoud Thabit Kombo 

Hayo yameelezwa na Waziri wa afya, Mahmoud Thabit Kombo wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Chake Chake Suleiman Sarhani aliyetaka kujua mchakato wa ununuzi wa mashine hiyo umefikia wapi.

Amesema ili  kufanikisha hilo tayari serikali imeshatangaza zabuni kwa ajili ya ununuzi wa mashine hiyo ambayo ni ya kisasa yenye uwezo mkubwa wa kutambua matukio mbali mbali ikiwemo vitendo vya ukatili wa kijinsia na ubakaji.

“Mheshimiwa Spika mashine hiyo itakuwa ni ya kisasa na ina uwezo wa kugundua au kukamua maji maji ya mtu aliyebakwa kwa muda wa wiki moja tokea kitendo kufanyika ikiwa hakusafishwa,” amesisitiza.

Amesema  tayari mkemia mkuu wa Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar amefanya safari nchini Kenya kwa ajili ya kuangalia sampuli ya mashine hiyo na kufanya mazungumzo na wakala wake.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search