DSE:Ukubwa mtaji kampuni za ndani wapanda bilioni mbili....soma habari kamili na matukio360....#share
Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
UKUBWA wa mtaji wa kampuni za ndani umepanda kwa Shilingi Bilioni 2 kutoka shilingi Trilioni 10.143 hadi kufika Shilingi Trilioni 10.145 wiki hii.
Mary Kinabo
Hali hiyo imetokana na kupanda kwa bei ya hisa ya SWISS kwa asilimia 1 na soko la hisa (DSE) kwa asilimia 1.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa habari mwandamizi Soko la Hisa (DSE) Mary Kinabo leo jijini Dar es Salaam inasema idadi ya hisa zilizo uzwa na kununuliwa kwa wiki iliyoishia februari 23, 2018 ni hisa milioni 3.3 ikilinganishwa na mauzo ya hisa ya milioni 11.6 kwa wiki iliyoishia tarehe 16 Februari 2018.
Amesema mauzo kwa wiki iliyoishia 23 Februari 2018 yalikuwa shilingi Bilioni 2.3 ikilinganishwa na mauzo ya shilingi bilioni 6.4 kwa wiki iliyoishia tarehe 16 Februari 2018.
Amefafanua kuwa ukubwa wa mtaji wa kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko umepanda kwa Shilingi Bilioni 456 kutoka Shilingi Trilioni 22.4 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 22.95 wiki iliyoishia februari 23, 2018.
"Ongezeko hilo limetokana na kupanda kwa bei za hisa za Kenya Comercial bank(KCB ) kwa asilimia 8, East African Breweries Ltd(EABL) kwa asilimia 7, soko la hisa (DSE) kwa asilimia 1 na Swissport(SWISS) kwa asilimia 1,"amesema.
Ameongeza kuwa Kiashiria cha kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimepanda kwa pointi 47 kutoka pointi 2,336 hadi 2,383 pointi hii ikiwa ni kutokana na kupanda kwa bei za hisa za Kenya Commercial Bank (KCB), East African Breweries Ltd (EABL), Swissport (SWISS) na Dar es Salaam Stock Exchange (DSE).
Amefafanua kuwa kishiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimepanda kwa pointi 1 kutoka pointi 3,868 hadi pointi 3,869 kutokana na kupanda kwa bei za hisa za Swissport (SWISS) na Dar es Salaam Stock Exchange (DSE).
"Kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) wiki hii imebaki kwenye wastani wa pointi 5286 kama wiki iliyopita.
"Kiashiria huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii imepanda kwa poniti 1 kutoka pointi 2,608 kadi pointi 2,609 hii imechangiwa na kupanda kwa bei za hisa za DSE kwa asilimia 1% kutoka shilingi 1580 hadi 1600,"amesema.
Ameongeza Kiashiria cha Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imepanda kwa pointi 2 kutoka pointi 2,462 hadi pointi 2,464 imechangiwa na kupanda kwa bei za hisa za SWISS kwa asilimia 1 kutoka shilingi 3500 hadi shillingi 3540.
Akizungumzia mauzo ya hati fungani Kinabo amesema katika wiki iliyoishia februari 23,2018 yalikuwa Shilingi bilioni 64 kutoka Shilingi Bilioni 8 wiki iliyopita ya februari 16,2018.
"Mauzo haya yalitokana na hatifungani kumi na sita (16) za serikali zenye jumla ya thamani ya Shilingi bilioni 68 kwa jumla ya gharama ya Shilingi bilioni 64,"amesema.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment