CUF wataka wazee, viongozi wa dini na wastaafu wakutane na Magufuli....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
CHAMA cha Wananchi CUF kimewataka wazee, viongozi
wa stahafu na viongozi wa dini akiwamo Kadinali Polycarp Pengo wamshauri na kumpa nasaha rais John
Magufuli arudi kwenye mstari ili kulinusuru taifa na mwelekeo mbaya
unaolikabili.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi CUF, Julius Mtatiro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Mwelekeo huo mbaya umetajwa kuwa ni kushamiri kwa mauji,
utekaji na mashabulizi, mashambulizi dhidi ya demokrasia, mihimili ya dola
kuwekwa mfukoni mwa serikali, hali ya uchumi wa nchi na kuvunjwa kwa haki na
kukithiri kwa vitendo vya upendeleo.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti
wa Kamati ya Uongozi wa CUF Julius Mtatiro alipokuwa akitoa taarifa zinazoeleza
kuwepo kwa mwelekeo mbaya wa taifa na kuishauri serikali.
“Taifa letu linao wazee, linao waasisi, linao viongozi
wastaafu. Kwa sababu mambo hayako sawa kwenye nchi yetu, wazee wetu Mwinyi,
Mkapa, Kikwete, Warioba, Butiku na wengine wote simameni na mwambieni JPM arudi
kwenye mstari,”
“Hakuna mtanzania ambaye angelipenda kupoteza muda wake
kumkosoa rais na serikali yake, lakini watanzania wanawajibika kufanya hivyo
kwa sababu ya maamuzi ya rais na utendaji wa serikali yake vinaathari za moja
kwa moja kawa maisha ya kizazi chetu na kijacho,” amesema na kuongeza Mtatiro.
Mauaji, utekeji na
mashambulizi
Mtatiro amesema kuwa vitendo hivyo kwa sasa nchini ni mambo ya
kawaida. Ameeleza kwamba matukio hayo leo yakutisha ya mauaji yamelitia madoa ya damu serikali lakini hadi sasa vyombo
vyenye dhamana havina majibu ya matukio hayo.
Mashambulizi dhidi ya
Demokrasia
Amesema tangu kuingia madarakani kwa uongozi wa serikali ya
awamu ya tano, kumekuwa na jitihada kubwa za kuua demokrasia na mfumo wa vyama
vingi hapa nchini na amedai kuwa juhudi hizo zinafanywa na rais Magufuli.
Mihimili ya dola
Kuwekwa mfukoni mwa serikali
Mwenyekiti huyo wakamati ya uongozi amedai kuwa mhimili mmoja
(serikali) umejipa mamlaka makubwa kiasi cha kudhibiti mihimili mingine. Ametoa
mfano kwa kusema serikali kwa sasa inapanga mipango mingi na inatumia fedha
nyingi za taifa bila kulihusisha bunge. Hivyo imelidhibiti bunge na mahakama
pia imedhibitiwa.
Hali ya uchumi wa nchi
Amedai, hali ya uchumi kwa sasa inaanguka kutokana na kwamba
mzunguko wa fedha ni mdogo, hali mbaya ya biashara, mfumuko wa bei za bidhaa za
vyakula na mabenki kufungwa, hivyo amesema kama hatua isipochukuliwa taifa
litaenda kubaya.
Kuvunjwa kwa haki na
kukithiri kwa vitendo vya upendeleo.
Amesema utawala wa awamu hii chini ya rais Magufuli unaongoza
taifa kwa kuwa na “double standard”, kujuana na upendeleo ambapo alitoa mfano
wa bamoa bomoa iliyowafanya kwa wakazi wa kimara jijini Dar es Salaam kwa madai
ya kuvamia hifadhi ya barabara huku juzi rais akisitisha bomoa bomoa kwa wakazi
wa Mwanza waliovamia eneo la uwanja wa ndige.
No comments:
Post a Comment