SMG tano, bastola tatu, risasi 47 zakamatwa....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Salha Mohamed, Dar es Salaam
JESHI la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam wamekamata watuhumiwa wawili wanaodaiwa kuhusika na kifo cha kada wa Chadema, Daniel John.
Pia limekamata silaha tano aina ya SMG, risasi 35, bastola tatu na risasi 12 katika matukio tofauti ya kiuhalifu. Na limemkamata Rajabu Mohamed 'Rajeshi' (25) kwa madai ya kuwakamata wanawake kwa kutumia nguvu na kuwanyang'anya vitu, kuwatisha kuwauwa kwa kuwanyonya damu au kuwakata sehemu za siri.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP, Lazaro Mambosasa (kushoto) akitoa taarifa ya Mtuhumiwa Rajabu Mohamed (25),mkazi wa Mwenge mwenye pingu aliyekuwa akifanya vitendo vya unyang'anyi kwa kutimia nguvu,ubakaji na udhalilishaji wa wanawake jijini humo
Vilevile limesema bado upelelezi dhidi ya mauaji ya mwanafunzi wa Chuo cha NIT, Akwilini Akwilina aliyefariki kwa kupigwa risasi wakati wa Maandamano unaendelea na kwamba ukikamilika wataweka wazi.
Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, SACP Lazaro Mambosasa amesema leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.
"Febuari 23,2018, meneo ya Hananasifu Kinondoni kufuatia uchunguzi unaoendelea juu ya mauaji walikamatwa watu wawili mmoja jinsia ya Kike na mwingine jinsia ya kiume kwa tuhuma zinazohusiana na mauaji ya Daniel, "amesema.
Amesema mtuhumiwa Rajabu amekamatwa kutokana na kuwakamata wanawake kwa kuwalaghai kuwa ni mfanyabiashara ambae hutumia gari lenye namba T 172 BLH Fun Cargo.
Amesema wakishaingia kwenye gari hutumia nguvu na kuwanyang'anya vitu vyao vilivyo ndani ya mabegi na kisha kuwazungusha barabarani huku akiwatisha kuwa yeye ni Freemason.
"Amekuwa akiwatisha kuwa yeye ni Freemason na na kuwa atawaua kwa kuwanyonya damu au kuwakata sehemu za miili yao.... Huwalazimisha watoe password ya simu zao na kuchukua kadi zao za bank na kuwaibia fedha kwenye ATM na baada ya hapo huwashusha na kuwatelekeza vichochoroni, "amesema.
Mambosasa amesema mtuhumiwa huyo amekiri kufanya vitendo hivyo na kuwataka wananchi waliofanyiwa vitendo hivyo na mtu huyo kutoa taarifa Polisi kwa ushahidi zaidi.
Ameongeza kuwa jeshi hilo limekamata silaha tano, SMG na risasi 35 ,bastola 3 na risasi 12 katika matukio tofauti ya kiuhalifu.
" Febuari 16,2018 Polisi lilipata taarifa ya kiintelijensia kuwa Chanika Homboza kuna kundi la wahalifu limepanga kufanya tukio la unyang'anyi wa kutumia silaha.
"Askari wakiwa njiani kuelekea eneo la tukio walikutana na kundi la watu zaidi ya sita na waliposimamishwa walikaidi amri na kuanza kufyatulia askari risasi na askari kujibu mashambulizi na hatimaye kuwazidi nguvu na kuwajeruhi watatu wengine wakikimbia, "amesema.
Amefafanua kuwa wahalifu hao wamefariki baada ya kuvuja damu nyingi na kwamba mmoja wa majeruhi hao walipopekuliwa alikutwa na SMG iliyofutwa namba ikiwa na risasi 28 ndani ya magazine na mwingine akiwa na silaha ndogo bastola aina ya Browning yenye namba TZ CAR 103143 ikiwa na risasi 9 ndani.
Akizungumzia makosa ya barabarani, Mambosasa amesema kuanzia Febuari 12/2018 hadi Febuari 23 /2018 wamefanikiwa kukusanya sh milioni 925 ikiwa ni tozo za makosa ya barabarani.
"Uvunjaji wa sheria barabarani bado ni mkubwa sana hivyo nawaasa wananchi ndani ya Kanda Maalum kuendelea kuheshimu sheria za barabarani, "amesema.

No comments:
Post a Comment