Madiwani Mufindi wapitisha bajeti bilioni 62.9 ....soma habari kamili na matukio360...share


Na Mwandishi Wetu, Mufindi 

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi limejadili, kuridhia na kupitisha rasimu ya bajeti yenye zaidi ya shilingi bilioni 62.926, ikiwa ni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka ujao wa Fedha 2018/2019, ambapo makusanyo ya ndani ya Halmashauri ni Bilioni 4.162 kati ya Fedha zote.


Sehemu ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya  Mufindi wakifuatilia Mjadala wa bajeti.

Akiwasilisha rasimu ya bajeti kwenye kikao maalum cha Baraza, kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Isaya Mbeje, amesema, Halmashauri inatarajia kukusanya, kupokea na kutumia zaidi ya shilingi Bilioni 62.926, ambapo kati ya fedha hizo Bilioni 40.728 ni fedha kutoka Serikali kuu maalum kwa ajili ya mishahara ya Watumishi, shilingi Bilioni 17.205 zimeelekezwa kwenye Miradi ya Maendeleo huku shilingi Bilioni 4.992 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo.

Mbenje ambaye pia ni ofisa Mipango wa Halmashauri, amevitaja vipaumbele vya bajeti hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019 kuwa inaangazia ukamilishaji wa miradi ambayo haikukamilika kwa miaka ya nyuma hususani ukamilishaji wa Majengo ya sekta ya ofya na Elimu, Ukarabati wa Madarasa chakavu ya baadhi ya Shule za Msingi, ukusanyaji Mapato kwa njia ya kielekroniki, Kutoa huduma bora za kijamii, kuinua uchumi wa wananchi na kuimarisha Miundombinu.

"Mwenyekiti rasimu hii ya Mpango wa Bajeti ya Halmashauri ni Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/2019, rasimu hii itaendelea kujadiliwa na kupatiwa ushauri kwenye vikao vya ngazi ya Mkoa, Ofisi ya Rais TAMISEMI Pamoja na Wizara ya Fedha na Mipango kablaya kujadiliwa na kupitishwa na Bunge,”amebainisha Mbenje.

Azungumza wakati wa kufunga kikao hicho, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mninga, Festo Mgina amewataka Madiwani kutoa ushirikiano kwenye zoezi la ukusanyaji wa mapato pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapoto ili yasaidie kuharakisha maendeleo kwa kuzingatia kuwa asilimia 60 Mapato ya ndani yanatakiwa kuelekezwa kwenye miradi ya Maendeleo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Festo Mgina akizungumza wakati wa kufunga kikao cha Baraza la Madiwani.


“Mkurugenzi wewe pamoja na timu yako tuendelee kuchapa kazi, tunasifa ya Ushirikiano kati ya timu ya Madiwani na Timu yako, tuendeleee kufanya kazi kwa umoja, uadilifu na ushirikiano Kwani sisi kama Viongozi tunatakiwa kuwa chachu ya Maendeleo,”amesema. 

Rasimu ya bajeti ya 2018/2019, ameandaliwa kwa kuzingatia, Ilani ya Chama cha tawala CCM, Mwongozo wa bajeti wa mwaka 2018/2019, Mpango wa pili wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/2017, Malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs), Dira ya Taifa

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search