Kingunge Kongambale Mwiru afariki dunia....soma habari kamili na matukio360....#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam

MWANASIASA mkongwe, Kingunge Kongambale Mwiru amefariki  dunia usiku wa kuamkia leo.

Rais Magufuli alipomjulia hali mzee Kingunge alipokuwa amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili

Ndugu wa karibu wa Kingunge ameiambia  matukio360 kuwa amefariki akiwa katika hospitali ya taifa ya rufani ya Muhimbili(MNH) alipokuwa amelazwa  akipatiwa matibabu kufuatia kung'atwa na kujeruhiwa na mbwa nyumbani kwake eneo la Victoria jijini Dar es salaam

Kifo hicho kinatokea ikiwa ni siku chache baada ya mke wake kufariki na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

Amefariki majira ya saa tisa usiku wa kuamkia leo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search