STARTIMES YAMKUTANISHA STAA WA UIGIZAJI KUTOKA NCHINI CHINA NA WASANII WA FILAMU NCHINI, SOMA HABARI KAMILI NA MATUKIO360..#SHARE

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KATIKA kuhakikisha wasanii wa Kitanzania wanapata maarifa katika utengenezaji wa Firamu zenye ubora,Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia bidhaa  yake ya StarTimes imewakutanisha muigizaji maarufu wa China Hai Qing maarufu kama Mau Dou Dou na wasanii wa Kitanzania pamoja na mashabiki wake kwa lengo la kujadilishana mbinu mbali mbali katika Sanaa za Uigizaji.

Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif (kulia) akimkabidhi tuzo Mwigizaji maarufu wa China, Hai Qing "Mau Dou Dou" (kushoto)  kwa niaba ya watanzania ambao ni mashabiki wake.

Hafla hiyo ya kuwakutanisha wasanii hao imefanyika  leo Jijini Dar es Salaam,katika ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (NICC) na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali maarufu ,pamoja na waandishi wa habari.

Mwigizaji huyu wa Kimataifa kutoka nchini China, Hai Qing maarufu kama Mau Dou Dou amekuja nchini Tanzania kwa ziara ya siku mbili pamoja na mambo mengine ni  kutangaza kampuni ya Startimes.

Akizungumzia ujio huo wa Mau Dou Dou,Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif amewaambia waandishi wa habari kuwa msanii huyo  sehemu kubwa anatangaza Kiswahili katika king’amuzi cha Startimes.

Amesema Kampuni ya StarTimes inatumbua mchango wa Lugha ya Kiswahili katika mawasiliano .

Amesema kuwa msanii huyo amekuwa na kazi nyingi kwa Ubalozi wa nchini China pamoja na Startimes ikiwa ni kukuza Kiswahili.

Katika Halfa hiyo ambayo kulikuwepo na wasanii mbali mbali wakiwemo Natasha, Yvone na Davina. 
.
Mwigizaji maarufu wa China, Hai Qing "Mau Dou Dou" (kushoto) akizungumza jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari, wasanii wa filamu nchini pamoja na mashabiki wake leo Jijini Dar es Salaam
Meneja Masoko na Mahusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Sharobaro(kulia) akifanya mahojiano na Mwigizaji maarufu wa China, Hai Qing "Mau Dou Dou"  alipokutana na wasanii wa filamu pamoja na mashabiki wake leo kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif (kulia) akimkabidhi tuzo Mwigizaji maarufu wa China, Hai Qing "Mau Dou Dou" (kushoto)  kwa niaba ya watanzania ambao ni mashabiki wake
Msanii wa filamu nchini Tanzania, Suzan Lewis "Natasha "(kulia) akitoa shukrani kwa niaba ya wasanii wa filamu nchini wakati wa ziara ya  Mwigizaji maarufu wa China, Hai Qing "Mau Dou Dou"  alipofika na kufanya mazungumzo nao leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wasanii wa Filamu nchini pamoja na mashabiki wa Mwigizaji maarufu wa China, Hai Qing "Mau Dou Dou"  wakifuatilia mada wakati wa mkutano huo.(picha kwa hisani ya Michuzi Media)


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search