UPDATES: Sugu, Masonga jela miezi mitano....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Mbeya
MAHAKAMA ya hakimu mkazi Mbeya leo imewatia hatiani Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi na katibu wa Chadema nyanda za juu kusini Emmanuel Masonga na kuwahukumu kifungoni cha miezi mitano jela


Wamehukumiwa kwa kosa la kumtumia lugha ya fedheha dhidi ya rais John Magufuli.  Hukumu imetolewa  na hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo , Michael Mteite.



Awali kabla ya hukumu ulinzi uliimarishwa katika Mahakama hiyo na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) 


Wawili hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30,2017 eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.
. 
Upande wa mashtaka na wa utetezi ulikamilisha ushahidi Februari 9,2018.

Jamhuri iliwasilisha mashahidi watano na kielelezo kimoja cha sauti iliyodaiwa kurekodiwa na shahidi wa tano, Inspekta Joram Magova.

Upande wa utetezi uliwasilisha mashahidi sita wakiwamo Sugu na Masonga waliokana kutamka maneno wanayoshtakiwa kuyatoa.
Washtakiwa walitetewa na mawakili Sabina Yongo, Boniface Mwabukusi na Hekima Mwasipu kabla ya kujitoa, hivyo sasa wanawakilishwa na Peter Kibatala.


Kwa mara ya kwanza, Sugu na Masonga  walifikishwa mahakamani Januari 16 na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mkuu, Joseph Pande aliyeeleza upelelezi ulikuwa umekamilika na walikuwa tayari kuendelea na usikilizaji

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search