Makonda awasaka waliopora mali za Bakwata Dar es salaam....soma habari kamili na matukio360....#share

Na Salha Mohamed, Dar es Salaam


MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amelitaka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania(BAKWATA) mkoani humo kumpa orodha ya maeneo ya baraza yaliyoporwa mkoani humo.


Pia amewataka wamuombee kwa M/Mungu ili aweze kuwasaidia watu na kupata haki zao.
Paul Makonda akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa majengo ya makao makuu ya Bakwata leo jijini Dar es salaam

Ameyasema hayo  leo jijini Dar es Salaam  alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa  makao makuu ya baraza hilo na shule yanayogharimu sh bilioni 4.5


"Ninaomba mniletee orodha  ya maeneo ya Bakwata ya Dar es Salaam yaliyoporwa nataka kushughulika nayo ambayo wajanja wajanja wameyaingilia, "amesema.


Amewahakikishia maeneo hayo yatapatikana ili waislamu wafanye mambo yao ya maendeleo.


Katika hatua nyingine Makonda  amewataka waumini wa madhehebu yote  nchini kuwathamini viongozi wao bila kusubiri kuombwa msaada.


Kwa upande wake Mufti wa Tanzania, Abubakar Zuberi amesema "Tunakuombea kwa Mungu... Awali Bakwata kulikuwa kunafitina ndani kwa ndani na nje pia ndiyo maana hakukuwa na maendeleo kwa miaka zaidi ya 50".


Amewataka waislamu wajitambue, wabadilike na kuacha mazoea na kutengeneza dhambi kwa kuweka vigenge kwa kufanya fitina.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search