Wakuu wa wilaya wapewa siku moja kujieleza kwa barua ....soma habari kamili na matukio360....#share.

Na mwandishi wetu Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amewaweka kikaangoni wakuu wa wilaya baada ya kuwaagiza kuandika barua za kujieleza kwa kushindwa kutekeleza agizo la serikali la kufikia asilimia 100 ya uwekaji harama mifugo na kwamba wasipende kumjaribu katika utendaji wa kazi.

Amos Makalla

Ametoa agizo hilo leo alipokutana na wakuu wa wilaya,
wakurugenzi, wenyeviti wa halmashauri katika ukumbi wa mikutano wa hospitali ya mkoa na kwmaba hilo ni agizo la wizara ya Kilimo na mifugo katika kufuatilia utekelezaji wa zoezi hilo.

"Mimi siwezi kumfukuza mtu kazi ila kipimo chake cha utendaji
kitajulikana wizarani nasikitishwa sana katika uendeshaji wa zoezi hilo katika moja ya halmashauri nimeusishwa kuwa nina mifugo jambo ambalo ni uongo mtupu,"amesema.

Pia amewatahadharisha wakuu wa wilaya kutowahusisha wakurugenzi wa halmashauri kuhusika kukwamisha zoezi hilo kwa kuwa hilo ni jukumu walilokabidhiwa wao ili kufikia malengo waliyopewa na serikali .


Amefafanua katika halmashauri zote, Mbeya Jiji imefanya
vizuri kwa kufikia asilimia 100, Kyela 84, Chunya 82, Mbarali
83, Mbeya vijijini 81, Busokelo 75 na Rungwe kushika nafasi ya mwisho kwa asilimia 27 wakati ndio inayozalisha maziwa kwa wingi.

Amesema wakuu wa wilaya wasipende kumjaribu katika utendaji wa kazi na kwamba kila mtu ana wajibu wa kulinda kibarua chake na ufike wakati kufanya kazi kwa kujituma na si kwa mazoea.

Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja amesema watendaji wa serikali wanapaswa kutambua majukumu yao na maagizo kutoka ngazi za juu na kwamba wasikumbushwe majukumu yao.

Amesema wanapaswa kumtumia vizuri mkuu wa mkoa katika
uwajibikaji na utekelezaji wa majukumu na si kumlazimisha kufanya maamuzi magumu.



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search