Nzige watishia viwanja vya mpira kombe la Dunia 2018...soma habari kamili na matukio360....#share

Na mashirika ya kimataifa
MAAFISA wa serikali nchini Urusi wametahadharisha kwamba huwenda nzige wakashambulia viwanja vya mpira wa miguu nchini humo na kuzua kashfa kubwa wakati wa Kombe la Dunia.
Moja ya viwanja vitakavyochezewa katika kombe la Dunia nchini Urusi mwaka huu
Pyotr Chekmarev amesema takriban hektari milioni moja za ardhi kusini mwa Urusi zimevamiwa na wadudu hao.
Volgograd, mji ambao England watachezea dhidi ya Tunisia mnamo 18 Juni, ni moja ya maeneo ambayo yameathiriwa.
"Tumejifunza kukabiliana na nzige, lakini tutakwepa vipi kutumbukia katika kashfa ya dunia kutokana na nzige mwaka huu?" amesema Chekmarev.
"Ulimwengu wote utafika hapa. Viwanja vya mpira wa miguu vimejaa majani. Nzige hupenda maeneo ambayo kuna majani na rangi ya kijani.
"Utawazuia vipi kufika eneo ambalo mpira unachezewa?" aliongeza Chekmarev, mkuu wa idara ya ukulima katika wizara ya kilimo.
Kombe la Dunia 2018 litaanza mnamo 14 Juni na mechi zitachezewa viwanja 12 katika miji 11 Urusi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search