Polisi Dar wapiga marufuku maandamano.... soma habari kamili na matukio360...#share
Na Salha Mohamed, Dar es Salaam
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku kufanya maandamano yanayohamasihwa kwenye mitandao ya kijamii na kupuuza taarifa hizo.
Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam baada ya kuona taarifa ya watu wanaohamasisha maandamano kwenye mitandao ya kijamii.
o.
"Yeyote atakayeshindwa kupokea haya ninayoyasema asijutie yatakayotokea. . Jeshi limesimama tupo imara na hatutaruhusu mtu yeyote kuvunja sheria,"amesema.
Amesema wanaoendelea kuhamasisha wananchi kuvunja sheria na kuwataka wajiandae kwa maandamano tarehe wanazoendelea kutaja hali ya kuwa wao wapo mahali salama wanataka kuwaingiza watanzania wengine kwenye shida.
"Mimi nawaona watanzania ambao siku zote wanajua thamani ya amani wajiepushe na uchochezi huo, wajiepushe na mpango wa watu wachache wa kutaka kuingiza nchi kwenye vurugu,"amesema.
Amesema wanatengeneza mazingira rafiki kuhakikisha jiji linakuwa salama ili wawekezaji waendelee kuwekeza mitaji yao na hata kuvuta wengine kuwekeza jijini humo.
"Wachache wanaotaka kutuondoa katika msimamo huo hawana bahati sisi tumesimama hatutaruhusu mtu, tutachukua hatua na tutamshughulikia kwa mujibu wa sheria naomba hilo lieleweke hivyo hakuna atakayerudi nyuma tumesimama kuhakikisha watanzania wanalindwa na Jeshi lao la Polisi, "amesema.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment