Kijana aliyeiba kiroba cha mahindi na kumnasia kichwani aachiwa huru...soma habari kamili na Matukio360... #share

MAHAAMA ya Mwanzo Mlandizi mkoani Pwani imemuachia huru, kijana Frank Joseph (23) aliyeiba kiroba cha Mahindi debe 1 na kumnasia kichwani baada ya mlalamikaji kutofika mahakamani hapo mara 3 mfululizo.

Frank ambaye ni mkazi wa Mbezi DSM, ameachiwa huru na Hakimu Mfawidhi, Nabwike Mbaba wakati shauri hilo lilipoitishwa kwa ajili mlalamikaji (mtendewa) kutoa maelezo ya jinsi alivyoibiwa.

Hakimu Mbaba amesema kuwa kutokana na mlalamikaji (mtendewa) kushindwa kufika mahakamani hapo mara 3 mfululizo kutoa maelezo ya kuibiwa kwake anaifuta kesi huyo.

“Mtendewa ameshindwa kufika mahakamani licha ya kupewa wito mara 3 mfululizo, hivyo naifutilia mbali kesi hii na mshtakiwa kuanzia sasa upo huru,” amesema Hakimu Mbaba.

Awali mshtakiwa alishindwa kufikishwa mahakamani mara 2 mfululizo kutokana na gari la Magereza kuharibika.

Katika kesi hiyo namba 124/2018 Frank anadaiwa kutenda kosa la wizi May 3, 2018 saa 7 usiku maeneo ya Mlandizi ambapo aliiba Mahindi debe 1 likiwa na thamani ya Sh.20, 000 ikiwa mali ya Seve Seleman.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search